Kuunda Programu Mpya

Programu zimegawanywa Katika kila taasisi kulingana na Shughuli tofauti zinazofanywa. zinaweza kuwekwa kulingana na shughuli zinazofanywa katika taasisi (tiba ya matamshi,mafunzo ya kiufundi n.k) au kulingana na awamu (awamu ya asubuhi,awamu ya mchana) au darasa(darasa la kwanza, darasa la pili n.k) Kila eneo linahitaji kuwa na angalau programu moja.Programu nyingi zinaweza kuwa chini ya eneo moja.

Mtu binafsi (au mwanafunzi) anaweza kusajiliwa katika Programu moja au nyingi.

Watumiaji walio na nafasi ya uwakala wa Provider Setup (Utoaji Suduma),na walio na nafasi ya utawala wana fursa ya kuunda,kusasisha na kufuta programu.

1. Bonyeza katika tabu ya Admin kutoka kwenye Dashboard.

2. Kutoka kwenye tabu ya Admin,bonyeza kwenye New/Mpya pembeni na Program.

3. Jaza kila nafasi katika Create New Program (Tengeneza Programu Mpya) kama inavyohitajika.

N:B: Nafasi zilizo na alama ya nyota nyekundu (*) ni za lazima kujazwa.

4. Weka Jina la programu kwenye sehemu ya Program Name (Jina La Programu).

5. Unapojaza aina ya programu kwenye Program Type (Aina Ya Programu), Utakutana na menyu ndefu iliyoteremka.Pitia menyu au tafuta aina ya programu inayokaribiana na kazi unayofanya

Pia kuna chaguo la Other (Nyingine) ambayo unaweza kutumia kama hutapata inayoendana na mahitaji yako.

6. Chagua Site (Eneo) sahihi (ambayo ulishaitengeneza kabla) kutoka kwenye menyu iliyoteremka ili kuunda programu katika eneo ndani ya akaunti yako ya Therap.

7. Mfumo utahitaji Program ID (Kitambulisho Cha Programu). Hii inaweza kuwa jina sawa na la programu yako,au kifupisho cha jina la programu,au mchanganyiko wa herufi na nambari utakazopenda.

Kumbuka: Program Code (kodi ya programu), Cost Center Number (Nambari ya malipo ya kituo) na Capacity (Uwezo) ni chaguo zisizo za wajibu kujazwa.

8. Primary Contact (Mawasiliano ya msingi) na Secondary Contact (Mawasiliano ya ziada) yote ni chaguo zisizo za lazima.Ukishakamilisha sehemu hizi,taarifa ya mawasiliano ya mtu uliyemuingiza itaonekana Kwenye fomu ya data ya mtu binafsi aliyesajiliwa katika programu.Taarifa hii pia itaonekana katika sehemu zingine na kwenye ripoti tofauti tofauti ndani ya mfumo.

Kumbuka: kwenye Phone (Simu) unatakikana uingize Kodi ya nchi yako bila ya alama ya kujumlisha.(Kwa mfano: 255 kwa Tanzania)kwenye boksi iliyo Kulia inayosema “Ext” na uingize namba za simu zilizosalia kwenye boksi iliyopo kushoto.

  • Kubonyeza kwenye kitufe cha Save iliyopo chini ya ukurasa,itahifadhi programu na kukupeleka kwenye ukurasa wa ‘Program List’ (orodha ya programu).
  • Kubonyeza kwenye kitufe cha Save and Create New (Hifadhi na Tengeneza Mpya) kwenye ukurasa huu,itakupeleka kwenye ukurasa wa kutengeneza programu ingine.
  • Kubonyeza kwenye kitufe cha Cancel (Batilisha) itasitisha oparesheni hiyo.
  • Kubonyeza kwenye kitufe cha Save and Add Individuals (Hifadhi na Ongeza Watu Binafsi) itakupeleka utakapowasajili watu binafsi kwenye programu hiyo(ikiwa umeshawaingiza watu binafsi (au wanafunzi) kwenye mfumo.

9. Baada ya kubonyeza kwenye kitufe cha Save (hifadhi) meseji ya mafanikio itaoneshwa.

 Share on WhatsApp

Related user guides