Kusasisha & Kufuta Programu

Watumiaji wenye nafasi ya uwakala wa Provider Setup (Utoaji Huduma) wana haki ya kuunda,kusasisha na kufuta Programu.

1.  Bonyeza kwenye tabu ya Admin kwenye Dashboard.

2. Bonyeza kwenye kiungo cha List (Orodha) pembeni na Program.

3. Kwenye ukurasa wa Program List (orodha ya programu) kutakuwa na orodha ya programu za taasisi yako. Programu Active (hai), Inactive (zisizokuwa hai) na zingine zote zinaweza kuchaguliwa kutoka kwenye chujio la Status(hali) ili ziangaliwe.kwa kawaida chujio litaonesha programu zilizohai tu.

Sasisha Programu:

4. baada ya kuchagua programu kutoka kwenye ukurasa wa Program List,ukurasa wa Update/Delete Program utajitokeza. Baada ya kufanya mabadiliko yanayohitajika,bonyeza kwenye kitufe cha Update chini ya ukurasa ili kuhifadhi masahihisho.

5. Baada ya kubonyeza kitufe cha Update ujumbe wa mafanikio utaonekana.

Kufuta Programu:

  • Watumiaji hawataweza kufuta programu Kama kuna mtu binafsi amesajiliwa au aliwahi kusajiliwa kwenye programu hiyo.
  • Watumiaji hawataweza kuona wala kutafuta programu zilizofutwa.

6. Bonyeza kwenye kitufe cha Delete (futa)chini ya ukurasa wa Update/ Delete Program(sasisha/ futa programu) ili kufuta programu.

7. Baada ya kubonyeza kwenye kitufe cha Delete(futa),ujumbe wa onyo utaonekana.bonyeza kitufe cha Yes (ndio)ili kufuta programu.

8. Baada ya kubonyeza kwenye kitufe cha Yes(ndio),ujumbe wa mafanikio utaonekana.

 Share on WhatsApp

Related user guides